MENEJA wa Chelsea, Guus Hiddink amedokeza kuwa Eden Hazard anatarajia kuendelea kubakia Stamford Bridge msimu ujao. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amekuwa nje ya uwanja kwa karibu miezi miwili kabla ya kurejea na kufunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu msimu huu katika ushindi wa mabao 4-1 waliopata dhidi ya Bournemouth katika Uwanja wa Vitality. Hazard alikuwa mmoja wa wachezaji walioachwa katika kikosi cha kwanza na Jose Mourinho kabla hajatimuliwa Chelsea Desemba mwaka jana na Real Madrid na Paris Saint-Germain zimekuwa zikiripotiwa kumfuatilia kwa karibu nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. Akihojiwa Hiddink amesema anaamini klabu na mchezaji wote wana furaha na anategemea nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 kuendelea kubakia Stamford Bridge msimu ujao.
No comments:
Post a Comment