MSHAMBULIAJI nyota wa Leicester City, Riyad Mahrez amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ambayo inatolewa na Chama cha wachezaji wa Kulipwa-PFA. Mahrez amefunga mabao 17 na kutengeneza mengine 11 katika mechi 34 za ligi alizocheza na kuisaidia Leicester kukaribia kutwaa taji la Ligi Kuu. Nyota huyo wa kimataifa wa Algeria alipigiwa kura ya kutwaa tuzo hiyo na wachezaji wenzake wa kulipwa. Kiungo wa Tottenham Hotspurs, Dele Alli mwenye umri wa miaka 20 yeye aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka chipukizi wakati mwanadada Izzy Christiansen anayekipiga Manchester City yeye ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa wanawake. Mwanadada Beth Mead mwenye umri wa miaka 20 anayekipiga Sunderland amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka chipukizi kwa wanawake.
No comments:
Post a Comment