NGULI wa soka wa Brazil na mshindi mara tatu wa Kombe la Dunia, Pele ametuma salamu zake za rambirambi kwa marehemu Johan Cruyff, akimuelezea nguli huyo wa Uholanzi kama mtu aliyebadilisha mchezo wa soka. Cruyff alifariki Machi 24 mwaka huu baada ya kuugua kwa kipindi kifupi na kuacha kumbukumbu ya kipekee katika soka mabyo kamwe haitaweza kusahaulika kirahisi. Nguli huyo aliiongoza Ajax Amsterdam kunyakuwa mataji matatu ya Ulaya akiwa mchezaji na pia kuisaidia Barcelona kunyakuwa taji hilo mwaka 1992 wakati akiwa kocha. Cruyff pia aliibuka mchezaji bora katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1974, akiwa na kikosi cha Uholanzi ambacho kilifungwa na Ujerumani Magharibi katika hatua ya fainali. Akihojiwa Pele amesema hana shaka kuwa Cruyff ni mmoja kati ya wachezaji waliobadilisha kabisa soka la Ulaya na alifanya hivyo akiwa na mchezaji na baadae kama kocha.
No comments:
Post a Comment