KLABU ya Manchester City imepangwa kucheza na mabingwa wa kihistoria Real Madrid katika ratiba ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopangwa leo. Hatua hiyo inamaanisha City wanaweza kukutana na meneja wao ajaye Pep Guardiola katika hatua ya fainali baada ya Bayern Munich kupangwa kucheza na dhidi ya Atletico Madrid katika nusu fainali nyingine. Guardiola anatarajiwa kuchukua nafasi ya meneja wa sasa City Manuel Pellegrini majira ya kiangazi. Mechi za nusu fainali zinatarajiwa kuchezwa Aprili 26 na Mei 4 kwa mechi za marudiano huku ile ya fainali ikipangw akuchezwa katika Uwanja wa San Siro Mei 28.
Kwa upande wa ratiba ya nusu fainali ya michuano ya Europa League, Villarreal watakwaana na Liverpool huku Shakhtar Donetsk wao wakipangw akucheza na Sevilla. Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa Aprili 28 kwa mechi za mkondo wa kwanza na zile za marudiano zitachezwa Mei 5 huku fainali ikitarajiwa kufanyika Mei 18 Basel, Uswisi.
No comments:
Post a Comment