MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Christian Benteke anataka kufanya mazungumzo na klabu hiyo kujadili mustakabali wake baada ya kumaliza msimu wake wa kwanza ambao haukua mzuri kama ulivyotegemewa. Benteke amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda klabu kadhaa katika kipindi cha kiangazi ikiwemo West Ham United baada ya kushindwa kung’aa akiwa Anfield akifunga mabao 10 katika mechi 42 za mashindano yote aliyocheza toka anunuliwe kwa kitita cha paudi milioni 32.5 kutoka Aston Villa. Kukiwa hakuna uwezekano wa kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao baada ya kufungw amabao 3-1 na Sevilla katika fainali ya Europa League juzi, Benteke amesema yeye sambamba na wachezaji wengine wana matumaini ya kuzungumza na Jurgen Klopp kuhusu mipango ya msimu ujao. Akihojiwa Benteke amesema anafahamu kuwa bado anatakiwa kuzoea mazingira na kwasababu msimu umemalizika anadhani sasa ni wakati wa kukaa chini ya Klopp na kujaribu kutafuta suluhisho kwa ajili ya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment