KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Kaka ndio mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu ya Marekani-MLS, akimzidi nyota wa kimataifa wa Italia Sebastian Giovinco na nahodha wa Marekani Michael Bradley kufuatia viwango vilivyotolewa jana. Kaka mshindi wa ballon d’Or ambaye anacheza katika klabu ya Orlando City ya Florida anakunja mshahara wa dola 7,167,500 akifuatiwa na Giovinco anayechukua dola milioni 7,115,556 huku Bradley yeye akichukua dola milioni 6.5. Wachezaji wenye majina makubwa waliojiunga na MLS katika miaka ya karibuni ndio wanafuatia akiwemo Steven Gerrard anayecheza Los Angeles Galaxy anashika nafasi ya nne kwa kupokea kiasi cha dola 6,132,500. Wengine ni nyota wa New York City FC Frank Lampard anayekunja dola milioni sita, Andrea Pirlo dola milioni 5.9 na David Villa dola milioni 5.6.
No comments:
Post a Comment