SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limetangaza kuwa wanataka kuongeza ukubwa wa hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kutoka timu nane mpaka 16 ifikapo mwaka 2017. Kauli hiyo imetolewa na rais wa CAF Issa Hayatou katika mkutano wa maofisa wa shirikisho hilo uliofanyika huko Mexico City na kuongeza kuwa mfumo huo mpya utakuwa ukichezwa kama ligi ndogo ambayo itahusisha makundi manne yenye timu nne. Toka kuwekwa mfumo huu wa sasa mwaka 1997, hatua hiyo ya makundi imekuwa ikichezwa kwa kuwa na makundi mawili yenye timu nne kila moja. Washindi kutoka katka makundi hayo ndio wataingia moja kwa moja hatua ya nusu fainali na baadae fainali ambazo zote zitapigwa kwa mikondo miwili. Hayatou pia amesema zawadi kwa michuano yote miwili itapandishwa kumfuatia mkataba mpya walioingia na vyombo vya habari na masoko ambao unakadiriwa kufikia dola bilioni moja. Kwasasa mshindi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika anapata kitita cha dola milioni 1.5 wakati Kombe la Shirikisho ni dola 660,000.
No comments:
Post a Comment