MENEJA wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho amesema anatarajia kurejea kibaruani tena mwanzoni mwa msimu ujao lakini hakudokeza ni klabu gani haswa atakayofundisha msimu ujao. Mourinho raia wa Ureno aliondoka Stamford Bridge Desemba mwaka jana baada ya kuanza msimu kwa kusuasua na toka wakati huo amekuwa akihusishwa na tetesi za kuchukua kibarua cha Louis van Gaal katika klabu ya Manchester United. Akihojiwa Mourinho amesema hakuna dili lolote alilosaini mpaka hivi sasa lakini ana uhakika kuwa mpaka ikifika Julai atakuwa tayari ameshapata kibarua. Mourinho aliongeza kuwa kwasasa bado anaendelea kufurahia mapumziko yake lakini wakati ukifika angependa zaidi kufundisha klabu za bara la Ulaya.
No comments:
Post a Comment