KIUNGO mahiri wa Liverpool, Philippe Coutinho ameendelea kutawala tuzo za klabu hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kutwaa tuzo nne ikiwemo ya mchezaji bora wa msimu. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil pia ameikwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu ambayo huchaguliwa na wachezaji wenzake huku bao lake katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Manchester United katika michuano ya Europa League likiteuliwa kama bao bora la msimu. Akihojiwa Coutinho alishukuru kupokea tuzo hizo na kuongeza kuwa zina maana kubwa kwake kwakuwa zimetokana na wachezaji wenzake. Nyota huyo aliongeza kuwa wiki ijayo watakuwa wakkabiliwa na mchezo wa fainali hivyo aliwataka wachezaji wenzake kuendeleza ushirikiano huo ili waweze kumaliza msimu kw taji. Kwa upande mwingine chipukizi Emre Can yeye ndio alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu anayeinukia.
No comments:
Post a Comment