MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino amesaini mkataba mpya ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka mwaka 2021. Meneja huyo mwenye umri wa miaka 44 raia wa Argentina, aliteuliwa kushika nafasi hiyo Mei mwaka 2014 kwa mkataba wa miaka mitano na kuingoza Spurs kushika nafasi ya tani katika msimamo wa ligi na kucheza fainali ya Kombe la Ligi katika msimu wake wa kwanza. Kukiwa kumebaki mechi moja msimu huu, Spurs wana uhakika wa kumaliza katika tatu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu. Akihojiwa Pochettino amesema wanaamini huo ni mwanzo kwani katika mipango yao wamepanga kwenda mbali zaidi hapo walipofikia msimu huu. Spurs walikuwa wakifukuzia taji la Ligi Kuu mpaka walipolazimishwa sare ya mabao 2-2 na Chelsea wiki iliyopita hivyo kuwafanya kutoa mwanya kwa wapinzani wao Leicester City kutwaa hilo.
No comments:
Post a Comment