KOCHA wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Marc Wilmots ameita kikosi cha wachezaji 24 atakaowatumia katika michuano ya Euro 2016 huku akimuacha beki wa Manchester City Vincent Kompany kutokana na majeruhi. Akihojiwa Wilmots amesema kumkosa nahodha wao Kompany ni pigo kubwa kwa kikosi chake kwani alikuwa kiongozi mzuri na kumuombea aendelee vyema na matibabu yake ili kurejea akiwa imara zaidi. Kocha huyo amemteua Eden Hazard kuwa nahodha katika kikosi hicho pamoja na winga huyo wa Chelsea kutokuwa na msimu mzuri. Majina mengine makubwa yaliounganishwa katika kikosi hicho ni pamoja na Kevin De Bruyne, Romelu Lukaku, Christian Benteke na Divock Origi. Ubelgiji wamepangwa kundi E sambamba na Italia, Sweden na Jamhuri ya Ireland na mchezo wao wa kwanza unatarajiwa kuwa dhidi ya Italia Juni 13.
Kikosi kamili cha Ubelgiji.
Makipa: Thibaut Courtois (Chelsea), Simon Mignolet (Liverpool), Jean-Francois Gillet (Mechelen)
Mabeki: Toby Alderweireld, Jan Vertonghen (Tottenham), Nicolas Lombaerts (Zenit st Petersburg), Jason Denayer (Manchester City, on loan at Galatasaray), Dedryck Boyata (Celtic), Bjorn Engels (Club Brugge), Jordan Lukaku (Oostende), Thomas Meunier (Club Brugge), Thomas Vermaelen (Barcelona)
Viungo: Axel Witsel (Zenit St Petersburg), Marouane Fellaini (Manchester United), Mousa Dembele (Tottenham), Radja Nainggolan (Roma)
Washambuliaji: Eden Hazard (Chelsea), Kevin De Bruyne (Manchester City), Romelu Lukaku (Everton), Dries Mertens (Napoli), Michy Batshuayi (Marseille), Christian Benteke, Divock Origi (Liverpool), Yannick Ferreira-Carrasco (Atletico Madrid)

No comments:
Post a Comment