MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amekubali kutupia lawama kufuatia kipigo cha mabao 3-1 walichopata kutoka kwa Sevilla katika mchezo wa fainali ya Europa League na kudai kuwa watarejea wakiwa imara zaidi. Liverpool walianza vyema mchezo huo kwa kuongoza lakini walijikuta wakipoteana katika kipindi cha pili na kuipa mwanya Sevilla kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushinda taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo. Kipigo hicho pia kinamaanisha Liverpool hawatashiriki michuano yoyote ya Ulaya msimu ujao. Akihojiwa Klopp ambaye alichukua mikoba ya kuinoa Liverpool Octoba mwaka jana, amesema kikosi chake kilicho kwa asilimia 50 mpaka 60 ya kiwango chao cha kawaida na wanatakiwa kukubaliana na hilo. Klopp aliongeza kuwa anawajibika kwa kikosi chake kucheza kwa kiwango hicho na kuahidi kuwa watatumia kama mfano ili wakirejea wawe imara zaidi.
No comments:
Post a Comment