MSHAMBULIAJI wa Deportivo La Coruna, Lucas Perez anadaiwa kuwa tayari kuachana na klabu hiyo kufuatia taarifa za kuwaniwa na klabu za Arsenal na Leicester City. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa katika kiwango kizuri toka ahamie Deportivo akitokea PAOK ya Uturuki baada ya kufunga mabao 17 katika mechi 35 za La Liga alizocheza mpaka sasa. Kufuatia hatua hiyo Perez amekuwa akiwindwa kwa udi na uvumba na vilabu mbalimbali kutoka Serie A na Ligi Kuu huku Leicester na Arsenal zilitajwa kupigana vikumbo. Maofisa wa klabu hiyo wamekuwa wakipambana kujaribu kumbakisha mchezaji huyo na inafahamika kuwa hataweza kuondoka kwenda klabu za Hispania Real Madrid au Barcelona.
No comments:
Post a Comment