MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema kikosi chake kinastahili kuwepo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wakijiandaa na mchezo wao wa mwisho wa msimu dhidi ya Swansea City. City watakwenda katika mchezo huo wakiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu na wanafuzu kushiriki michuano hiyo pale tu watakaposhinda katika Uwanja wa Liberty. Pellegrini ambaye ataondoka City baada ya msimu kumalika, anadhani wachezaji wake wanastahili nafasi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa kwa vilabu Ulaya na kueleza kujivunia kwa mafanikio aliyopata katika kipindi cha miaka mitatu Etihad. Akihojiwa Pellegrini ambaye ameshinda taji moja la Ligi Kuu na mawili ya Kombe la Ligi amesema anajivunia mafanikio aliyopata City kwani klabu hiyo imekuwa ikua kila mwaka. Pellegrini aliongeza kuwa pamoja na kwamba anaondoka lakini anataka kuhakikisha wanashiriki michuano ya Ulaya mwakani kwani wanastahili hilo.
No comments:
Post a Comment