CHAMA cha Soka cha Jamhuri ya Czech-FACR jana kimewafungia waamuzi wawili ambao walionekana wakiwa wamelewa uwanjani wakati wa mchezo wa Ligi Kuu kati ya FK Pribram na Slavia Prague. FACR imedai kuwa waamuzi hao Marek Pilny na mwamuzi msaidizi Jiri Jech wanaweza kupoteza leseni zao na kukabiliwa na mashitaka ya kinidhamu. Chama hicho kimesema Pilny alionekana wazi akiwa amelewa kuanza mwanzo wa mchezo huo uliofanyika Jumatano kutokana na kushindwa kujimudu na kuanguka mpaka kufikia hatua ya kusaidiwa na mlinzi. Pilny alichezesha mchezo huo mpaka muda wa mapumziko lakini alitimka kabisa na kutorudi pindi alipoenda katika vyumba vya kubadilishia nguo. Kwa upande wa Jech naye pia aling’amuliwa kuwa amelewa kwa kushindwa kujizuia na kwenda kujisaidia haja ndogo wakati wa mchezo.
No comments:
Post a Comment