Monday, May 23, 2016

MESSI ADAI MSIMU HUU WALIPAMBANA SANA KUPATA MAFANIKIO.



MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amedai kuwa walilazimika kupambana ili kuhakikisha wanatetea mataji yao mawili ya nyumbani msimu huu. Barcelona walifanikiwa kutwaa taji la Kombe la Mfalme kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sevilla na kuijiongezea taji lingine baada ya lile la La Liga ambayo walilinyakuwa siku ya mwisho wa ligi. Katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Vicente Calderone Barcelona ilishuhudia kiungo wake Javier Mascherano akitolewa nje kwa kadi nyekundu kabla ya mapumziko lakini mabao ya Jordi Alba na neymar ambayo yalitengenezwa na Messi yalitosha kuwapa ushindi huo. Messi aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wao kijamii wa Facebook kuwa ubingwa wao wa safari haukuja kirahisi lakini juhudi zao za kucheza kwa umoja na kupambana kwa bidii kuliwasaidia kupata mataji hayo. Kombe la Mfalme linakuwa taji nne kwa Barcelona msimu huu baada ya kutwaa taji la Super Cup la UEFA na klabu bingwa ya dunia mwishoni mwa mwaka jana.

No comments:

Post a Comment