NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na James Rodriquez wanatarajiwa kuikosa michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu nchini Brazil. Ronaldo nahodha wa Ureno na Rodriguez anayeiwakilisha Colombia wote hawatarajiwi kuteuliwa katika vikosi vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo kwasababu ya ushiriki wao katika michuano ya Euro 2016 na baadae Copa America. Kocha wa kikosi cha Olimpiki cha Ureno Rui Jorge amesema pamoja na kwamba hajafanya maamuzi ya wachezaji gani waliozidi umri wa miaka 23 atakaowatumia katika michuano hiyo lakini hadhani kama Ronaldo atakuwa mmoja wapo. Kwa upande wa Rodriquez, rais wa Chama cha Soka cha Colombia, Ramon Jesurun amesema tayari nyota huyo ameshafanya maamuzi kuwa atacheza Copa America badala ya Olimpiki.
No comments:
Post a Comment