Wednesday, June 22, 2016

COPA AMERICA 2016: ARGENTINA YATINGA FAINALI KWA KISHINDO, MESSI AVUNJA REKODI.



MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi amekuwa mfungaji anayeongoza kwa nchi hiyo baada ya kuibamiza Marekani kwa mabao 4-0 na kutinga fainali ya michuano ya Copa America mapema leo. Nyota huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 28, aliipita rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Argentina Gabriel Batistuta ya mabao 54, kwa bao murua la mpira wa adhabu alilofunga katika mchezo huo. Mbali na kufunga bao hilo Messi pia alitoa pasi ya bao la kuongoza lililofungwa na Ezequiel Lavezzi huku mengine mengine mawili yakifungwa na Gonzalo Higuain. Akihojiwa Messi ambaye Ijumaa hii anatimiza miaka 29, amesema amefurahi kuifikia na kuipita rekodi ya Batistuta na kuwashukuru wachezaji wenzake kwakuwa wanastahili pia kutokana na mchango wao. Argentina sasa wanatarajiwa kucheza na aidha Colombia au mabingwa watetezi Chile ambao watapambana Afajiri ya kesho huko Chicago.

No comments:

Post a Comment