Sunday, June 26, 2016

COPA AMERICA 2016: COLOMBIA WATWAA NAFASI YA TATU.



MSHAMBULIAJI nyota wa AC Milan, Carlos Bacca alifunga bao pekee wakati Colombia ilipowachapa wenyeji Marekani kwa bao 1-0 ba kutwaa nafasi ya tatu ya michuano ya Copa America mapema leo. Bacca mwenye umri wa miaka 29 alifungwa bao hilo la ushindi katika dakika 31 ya mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Phoenix huko Glendale, Arizona. Hii ni mara ya pili kwa Colombia kuwafunga Marekani katika michuano hiyo baada ya pia kufanya hivyo katika mchezo wao wa ufunguzi ambao walishinda mabao 2-0. Mchezo wa fainali ya michuano hiyo unatarajiwa kupigwa Alfajiri ya kuamkia kesho ambapo Argentina watakwaana na mabingwa watetezi Chile huko East Rutherford, New Jersey.

No comments:

Post a Comment