Tuesday, June 7, 2016

DI MARIA AMLILIA BIBI YAKE.

SAA chache baada ya kugundua bibi yake amefariki, Angel Di Maria alikuwa akifikiria jinsi gani bibi yake huyo angekasirika kama asingeichezea Argentina katika mchezo wa ufunguzi wa Copa America dhidi ya Chile. Akihojiwa Di Maria amesema kama hachezi mpira bibi yake huwa anakasirika sana.  Katika usiku ambao nyota wa Argentina Lionel Messi alikosekana kutokana na majeruhi ya mgongo, Di Maria alibeba vyema jahazi la nchi yake kwa kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 51 kabla ya kumsaidia Ever Banega kufunga lingine la pili katika ushindi wa mabao 2-1 waliopata. Baada ya kufunga bao hilo, nyota huyo anayekipiga katika klabu ya Paris Saint-Germain alishikilia fulana iliyokuwa na na maandishi ya kumkumbuka bibi yake. Di Maria ambaye ndio walikuwa mchezaji bora wa mchezo huo, aliendelea kudai kuwa ni vigumu vitu kama hivyo vikitokea wakati uko mbali lakini mama yake alimsisitiza abakie na wachezaji wenzake ili kuhakikisha wanshinda mchezo.

No comments:

Post a Comment