Tuesday, June 7, 2016

NEYMAR ATAKIWA KUSHITAKIWA KWA UDANGANYIFU.

WAENDESHA mashitaka nchini Hispania wametaka mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Barcelona, Neymar ashitakiwe kwa kosa la udanganyifu. Waendesha mashitaka hao kutoka mahakama ya juu ya makosa ya jinai ya Hispania, wanamtuhumu Neymar na baba yake kuficha ukweli wa thamani halisi ya uhamisho wake kutoka Santos kwenda Barcelona. Barcelona ilitangaza kumnunua Neymar kwa kitita cha euro milioni 57 mwaka 2013, huku wazazi wake, Neymar da Silva Santos na Nadine Goncalves sa Silva Santos wakipaya euro milioni 40 na klabu yake ya zamani Santos wakipata euro milioni 17. Lakini waendesha mashitaka hao wamesema ada ya uhamisho ya nyota huyo ilifikia euro milioni 83 ingawa pande zote mbili zimekanusha kufanya jambo lolote baya kwenye uhamisho huo.

No comments:

Post a Comment