Thursday, June 16, 2016

DORTMUND YANASA BEKI LA LORIENT LILILOKUWA LIKIWINDWA NA BARCELONA NA LIVERPOOL.

KLABU ya Borussia Dortmund inadaiwa kukamilisha usajili wa Raphael Guerreiro kutoka Lorient baada ya beki huyo kukubali kusaini mkataba wa miaka minne Signal Iduna Park. Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 amecheza mechi 102 za Ligue 1 akiwa na Lorient katika kipindi cha miaka mitatu na kuna tetesi kuwa alikuwa akiwindwa pia na Barcelona na Liverpool. Lakini Dortmund walithibitisha kushinda mbio hizo mapema leo kwa kitita kinachodaiwa kuwa euro milioni 12. Usajili huo umemfanya mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Michael Zorc kuwa furaha baada ya kuwa tayari wameshanasa saini za Marc Bartra, Ousmane Dembele, Mikel Merino, Emre Morn a Sebstian Rode. Akihojiwa Zorc amesema Guerreiro ni mchezaji mwenye kipaji na ufundi wa hali ya juu ambaye anaweza kucheza nafasi kadhaa uwanjani hivyo wanafurahia kwa kuichagua Dortmund.

No comments:

Post a Comment