BEKI wa Liverpool, Martin Skrtel anadaiwa kukaribia kumalisha uhamisho wake kwenda klabu ya Fenerbahce ya Uturuki. Fenerbahce ilitenga ofa ya paundi milioni 5.5 kwa ajili ya beki huyo na Liverpool wamekubali ofa hiyo kutokana na Skrtel kutokuwa katika mipango ya Jurgen Klopp kwa msimu ujao. Skrtel mwenye umri wa miaka 31 alianza katika mechi nne kwa Liverpool baada ya Januari kufuatia kuumia katika mchezo dhidi ya Watford Desemba mwaka jana. Ujio wa beki wa kimataifa wa Cameroon, Joel Matip kutoka Schalke kunaongeza ushindani wa nafasi katika safu ya ulinzi na Liverpool sasa wako tayari kumuachia Skrtel baada ya kukaa miaka nane Anfield. Skrtel ambaye kwasasa ndio nahodha wa Slovakia katika michuano ya Ulaya inayoendelea huko Ufarnsa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Fenerbahce pindi atakapomaliza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment