MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Barcelona na Chelsea, Samuel Eto’o jana amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Georgette Tra Lou katika sherehe iliyokuwa ya kuvutia. Nyota huyo wa zamani wa Cameroon alifanya harusi yake hiyo huko Stezzano, Italia na kuhudhuriwa na mamia ya watu.
Eto’o mwenye umri wa miaka 35 ambaye alicheza misimu miwili katika Serie A akiwa na Inter Milan kabla ya kwenda kucheza kidogo Sampdoria, alionekana akiwa maridadi katika suti ya rangi ya udhurungi wakati akishuka katika gari kuelekea kanisani.
Georgette Tra Lou ambaye ni mama wa watoto wawili wa Eto’o, alionekana katika picha akiwa katika gari la wazi la kifahari akielekea kanisani kwa ajili ya ndoa yake.
Miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria harusi hiyo ni pamoja na mchezaji mwenzake wa Barcelona Carles Puyol ambaye alikwenda akiwa na mkewe. Mwaka 2007 Eto’o na Georgette walifunga ndoa ya kimila nchini kwao Cameroon, nah ii ndio ilikuwa ndoa yao ya kwanza kanisani.

No comments:
Post a Comment