KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema hataweza kukipigia magoti Chama cha Soka cha nchi hiyo-FA ili kimuongeze mkataba mpya baada ya michuano ya Ulaya inayoendelea nchini Ufaransa. Mkataba wa Hodgson unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa michuano hiyo na mwenyekiti wa FA Greg Dyke amesema kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 atabakia endapo kama Uingereza itafanya vyema nchini Ufaransa. Akihojiwa kuelekea mchezo wao wa haua ya mtoano utakaofanyika kesho dhidi ya Iceland, Hodgson amesema atakuwa tayari kuendelea kuinoa timu hiyo kama FA watamtaka afanye hivyo lakini kamwe hatawapigia magoti. Uingereza ilianza michuano hiyo kwa sare ya 1-1 dhidi ya Urusi kabla ya kwenda kuifunga Wales mabao 2-1 na kuja kutoa sare ya bila kufungana na Slovakia katika mechi zao za kundi B, matokeo mbayo yaliwafanya kumaliza katika nafasi ya pili. Uamuzi wa Hodgson kufanya mabadiliko sita katika kikosi chake kwneye mchezo dhidi ya Slovakia ulikosolewa vikali na wadau mbalimbali huku kukiwa na taarifa kuwa uliwaudhi viongozi wa FA.
No comments:
Post a Comment