KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Kaka ametemwa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya michuano maalumu ya Copa Amerika kutokana na matatizo ya misuli. Shirikisho la Soka la Brazil lilithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa nafasi yake sasa itashikiliwa na nyota wa Sao Paulo, Ganso. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 anayekipiga katika klabu ya Orlando City SC alikuwa ameitwa katika kikosi hicho kuchukua nafasi ya winga wa Bayern Munich Douglas Costa aliyeumia wiki iliyopita lakini sasa nay eye anajikuta akiondolewa ikiwa zimepita siku tano toka aitwe. Mkurugenzi wa ufundi wa Brazil, Golmar Rinaldi amesema Kaka alionyesha kutokuwa fiti mazoezini na baada ya kumfanyia vipimo akaonyesha anahitaji kupumzika siku 20 bila kufanya mazoezi ndio maana wakamua kumuacha.
No comments:
Post a Comment