Thursday, June 2, 2016

LIVERPOOL YAKARIBIA KUMNASA CHIPUKIZI WA UTURUKI.

KLABU ya Liverpool inadaiwa kuongoza mbio za kumuwania chipukizi wa kimataifa wa Uturuki na klabu ya Nordsjaelland, Emre Mor. Mor mwenye umri wa miaka 18, anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora wanaochipukia Ulaya kwasasa baada ya kuonyesha kiwango bora katika Ligi Kuu ya Denmark na kumfanya kuitwa katika kikosi cha Uturuki kwa ajili ya michuano ya Euro 2016. Klabu za Manchester United, Borussia Dortmund na Ajax Amsterdam zinadaiwa pia kumuwania chipukizi huyo anayecheza nafasi ya kiungo wa kushambulia lakini Liverpool ndio wanadaiwa kuongoza katika kinyang’anyiro hicho. Mor amefunga mabao mawili na kusaidia mengine mawili mechi 13 alizoichezea klabu yake msimu huu.

No comments:

Post a Comment