Thursday, June 2, 2016

PELE AZIPIGA BEI MEDALI ZAKE ILI APATE FEDHA ZA MISAADA.

NGULI wa soka wa Brazil, Pele amesema ameweka mnadani zaidi ya zawadi zake 2,000 zikiwemo medali tatu za dhahabu za Kombe la Dunia na moja mfano wa taji la Jules Rimet ili aweze kukusanya fedha kwa ajili ya kutoa msaada na kwenda katika klabu yake ya zamani ya Santos. Mnada huo wa siku tatu ambao umefunguliwa Jumanne jijini London, unatarajiwa kuwa na vitu vyote vya kumbukumbu vya nguli huyo mwenye umri wa miaka 75 wakati akiitumikia Brazil, Santos na New York Cosmos na inadaiwa anaweza kukusanya zaidi ya dola milioni moja. Akihojiwa Pele ambaye anatajwa kama mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea duniani, amesema uamuzi wa kufanya hayo ni kusaidia watoto yatima wa Brazil. Pele aliendelea kudai kuwa nusu ya fedha atakazopata zitakwenda kusaidia hospitali ya watoto na sehemu zingine zinazohitaji msaada na kumbukumbu zake zingine zitakazobakia zitakwenda katika klabu yake ya Santos kwa ajili ya maonesho.

No comments:

Post a Comment