KLABU ya Manchester City inadaiwa kujipanga kumuwania mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang. City wana matumaini ya kumsana nyota huyo wa kimataifa wa Gabon mwenye umri wa miaka 26 katika kipindi hiki cha kiangazi. Aubameyang anatajwa kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora Ulaya baada ya kuonyesha kiwnago kikubwa Dortmund akifunga mabao 39 katika mashindano yote msimu uliopita. Meneja mpya wa City Pep Guardiola anafahamu vyema kipaji cha Aubameyang na ameona kuwa anaweza kumfaa katika mipango yake ya baadae. City wanadaiwa kuwa tayari kumsaidia Guardiola katika usajili kwa kujiandaa kuvunja rekodi ya usajili kwa kumleta nyota huyo Etihad.
No comments:
Post a Comment