SHIRIKISHO la Soka nchini Nigerina-NFF limethibitisha kuwa mchezaji na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo Stephen Keshi amefariki dunia kiwa na umri wa miaka 54. Nahodha huyo wa zamani wa Super Eagles, ni mmoja kati ya watu wawili kuwahi kushinda taji la michuano ya Mataifa ya Afrika akiwa mchezaji na kocha. Keshi pia amewahi kuinoa Togo na Mali na enzi zake wakati akicheza soka aliwahi kucheza katika klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji. Taarifa zinadai kuwa Keshi alifariki dunia ghafla kwa kile kinachodhaniwa kuwa shinikizo la moyo. Akiwa mchezaji Keshi alikuwa sehemu ya kikosi cha Super Eagles kilichotwaa taji la Mataifa ya Afrika mwaka 1994 na mwaka huohuo wakikaribia kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia. Akiwa kocha Keshi aliiongoza Nigeria kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2013 huku pia akifanikiwa kuifikisha timu hiyo katika hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 iliyofanyika nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment