MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi amewasili katika mahakama ya Barcelona kutoa ushahidi wake katika kesi ambayo yeye na baba yake Jorge wanatuhumiwa kukwepa kodi katika kipindi cha mwaka 2007 na 2009. Wawili hao wanatuhumiwa kukwepa ya zaidi ya euro milioni nne ya haki za matangazo ya picha kwa kutumia kampuni yenye unafuu wa kodi huko Belize na Uruguay. Wakati waendesha mashitaka nchini Hispania wakitaka kutolewa kwa fainali kali na kifungo jela, Messi na baba yake wamekanusha kufanya jambo lolote baya huku mawakili wa Messi wakisisitiza kuwa nyota huyo hajawahi kutumia hata dakika moja kusoma miakataba yake. Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa Jumanne inatarajiwa kumalizika leo huku hukumu yake ikitarajiwa kusomwa wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment