RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesema Neymar anatarajiwa kusaini mkataba mpya katika kipindi cha siku chache zijazo. Mkataba wa sasa wa neymar unamalizika Juni mwaka 2018 na mazungumzo ya mkataba mpya yamekuwa yakindelea kwa muda sasa hivyo kuzusha tetesi kuwa klabu za Real Madrid, Paris Saint-Germain au Manchester United zinaweza kulipa kitenzi cha euro milioni 200 kilichowekwa katika mkataba wake. Hata hivyo, akiongeza na wanahabari mapema leo, Bartomeu amesema Neymar hatakwenda popote na katika siku chache zijazo atasaini mkataba mpya wa miaka mitano zaidi. Wakala wa zamani wa Neymar, Wagner Ribeiro hivi karibuni alidai kuwa kuna klabu tatu kubwa zinazomfukuzia nyota huyo wa kimataifa wa Brazil lakini mwenyewe anafurahia kuendelea kubakia Camp Nou. Neymar alijiunga na Barcelona akitokea Santos mwaka 2013 a kufanikiwa kushinda taji la La Liga na Kombe la Mfalme mara mbili pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana.
No comments:
Post a Comment