MWAMUZI kiongozi wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Pierluigi Collina amesema beki wa Hispania Sergio Ramso alipaswa kuruhusiwa kurudia penati yake dhidi ya Croatia Jumanne iliyopita baada ya kipa Danijel Subasic kutoka katika mstari wake mapema. Collina amekiri ilikuwa sio sawa kwa mwamuzi Bjorn Kuipers kumruhusu Subasic kutoka katika mstari wake mapema na kwenda kuokoa penati ya Ramos. Kukosa kwa penati hiyo kulifanya matokeo kubaki sare ya bao 1-1 kabla ya Croatia hawajakwenda na kuongeza lingine na kuwafanya waongoze kundi lao na kuifanya Hispania kwenda kukwaana na Italia katika hatua ya mtoano. Akihojiwa Collina amesema baada ya timu ya waamuzi kupitia mchezo huo waling’amua makosa ya wazi kwa kipa huyo aliyesogea mbele hivyo haukuwa uamuzi sahihi. Kuelekea hatua ya mtoano ambapo penati zinanafasi kubwa katika mechi hizo, Collina amesema watafanya jitihada kuhakikisha makosa hayo hayajirudii tena.
No comments:
Post a Comment