WAZIRI mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi amesema ameiuza klabu ya soka ya AC Milan kwa kampuni kutoka China. Berlusconi ambaye anaimiliki klabu hiyo ya Serie A, alitoa kauli hiyo katika gazeti moja nchini humo jana. Berlusconi amesema kampuni hiyo italipa kiasi cha euro milioni 400 katika kipindi cha miaka miwili ijayo, ambapo thamani hiyo inaweza kupanda mpaka kufikia euro milioni 750 pamoja na madeni. Hata hivyo, Berlusconi hakutaja ni kapuni gani haswa iliyoinunua klabu hiyo kwa madai kuwa bado kuna baadhi ya vitu havijamalizika. Berlusconi mwenye umri wa miaka 79, aliwahi kuwa waziri mkuu kwa vipindi vine lakini alihukumiwa kwa masuala ya ufisadi na rushwa.
No comments:
Post a Comment