MENEJA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema Jose Mourinho hakufanya uamuzi sahihi kwa kuchagua kurejea kuiongoza Chelsea kwa mara ya pili. Baada ya kuinoa Chelsea kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007, Mourinho alirejea tena Stamford Bridge mwaka 2013 na kushinda taji la Ligi Kuu lakini hakudumu sana kwani alitimuliwa Desemba mwaka jana baada ya timu hiyo kusuasua. Lakini sasa amepata kibarua kipya Old Trafford ambapo Ferguson amekuwa nguli kwa kipindi cha zaidi ya miaka 26 aliyoinoa United. Akihojiwa Ferguson alimuunga mkono rafiki yake huyo kuwa atafanikiwa katika klabu yake hiyo mpya lakini alikosoa uamuzi wake wa kurejea Chelsea.
No comments:
Post a Comment