MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uingereza, Harry Kane anadaiwa kukaribia kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu ya Tottenham Hotspurs. Kane mwenye umri wa miaka 22, amefunga mabao 25 na kufanikiwa kutwaa kiatu cha dhahabu katika msimu wa 2015-2016, lakini alishindwa kung’aa katika michuano ya Ulaya akiwa na Uingereza. Nyota huyo alikuwa amesaini mkataba mpya wa kuongezwa mshahara na kufikia paundi 50,000 Februari mwaka huu lakini sasa makubaliano mapya yanamfanya aendelee kuitumikia timu hiyo mpaka mwaka 2021. Spurs pia wanadaiwa kuwa karibu kumsajili mshambuliaji wa AZ Alkamaar ya Uholanzi, Vincent Jansse huku dili hilo likitarajiwa kukamilika wiki hii.
No comments:
Post a Comment