UWANJA wa Allianz Arena uliopo jijini Munich jana ulipambwa kwa rangi nyekundi, nyeupe na bluu tofauti na rangi nyeupe iliyozoeleka wakati Bayern Munich wakisherekea Siku ya Uhuru ya Marekani kwa kuwasha taa katika uwanja zikiwa na rangi ya bendera la taifa hilo. Bayern pia walitumia nafasi hiyo kutambua klabu rasmi 100 za mashabiki zilizoko nchini Marekani. Klabu hiyo ilifungua ofisi zake jijini New York mwaka 2014 na kushuhudia klabu za mashabiki kukua kutoka vikundi nane mwaka 2014 mpaka kufikia 100 hivi sasa. Mabingwa hao wa Bundesliga wanatarajiwa kuanza ziara kiangazi hiki nchini Marekani, wakitarajiwa kupita katika miji ya Chicago, Charlotte, North Carolina na New York kwa ajili ya Kombe la Ubingwa wa Kimataifa.
No comments:
Post a Comment