KLABU ya Monaco imefanikiwa kunasa saini ya Kamil Glik kutoka klabu ya Torino kwa dili linaloaminika kufikia euro milioni nane. Beki huyo wa kati alikaririwa hivi karibuni akidai kuwa anakaribia kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligue 1 na sasa kauli yake hiyo imetimia. Nyota huyo wa kimataifa wa Poland amesaini mkataba huo na Monaco ambao utamalizika mwaka 2020, baada ya kuisaidia nchi yake kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya ambapo walifungwa na Ureno kwa matuta. Akihojiwa Glik amesema amefurahi kusajiliwa na Monaco kwani ni klabu kubwa nchini Ufaransa na itamsaidia kuimarika zaidi kuliko alivyokuwa awali.
No comments:
Post a Comment