Saturday, July 9, 2016

BARCELONA WAANZISHA KAMPENI YA KUMUUNGA MKONO MESSI.

KLABU ya Barcelona imeanzisha kampeni ya kuwataka mashabiki wao kuonyesha huruma yao kwa kumuunga mkono mshambuliaji wao nyota Lionel Messi baada ya kukata rufani kupinga adhabu ya kifungo cha miezi 21 jela kwa kosa la ukwepaji kodi. Messi na baba yake Jorge walitolewa hukumu hiyo Jumatano iliyopita baada ya mahakama ya Barcelona kuwakuta na hatia ya makosa matatu likiwemo la ukwepaji kodi inayokadiriwa kufikia euro milioni 4.1. Timu ya mawakili wa Messi ilidai jana kuwa wawili hao wanatarajia kukata rufani mahakama kuu, pamoja na kwamba hakuna yeyote atakayelazimika kukaa jela. Chini ya sheria za Hispania, kifungo chochote chini ya miaka miwili huwa mtuhumiwa anakuwa hana hata ya kwenda kukitumikia jela, hata hivyo klabu hiyo imewataka mashabiki wake kupaza sauti zao ili kumuunga mkono shujaa wao katika mitandao ya kijamii. Mbali na kifungo hicho, lakini pia Messi alitozwa faini ya euro milioni mbili wakati baba yake akilimwa faini ya euro milioni 1.5.

No comments:

Post a Comment