KOCHA Marcelo Bielsa ametupia lawama uamuzi wake wa kujiuzulu Lazio kwa rais wa klabu hiyo, akidai kuwa ahadi ya usajili ilishindw akutekelezwa. Bielsa alitangazwa meneja mpya wa Lazio mapema wiki hii lakini alijiuzulu muda mfupi baadae na kuzua taharuki kuwa anaweza kushitakiwa. Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa Marseille, Athletic Bilbao, Chile na Argentina alitetea uamuzi huo na kuamua kuelezea sababu zake. Bielsa amesema yeye na wenzake walifikia uamuzi huo baada ya klabu hiyo kushindwa kusajili mchzaji yeyote kati ya waliowapendekeza jambo ambalo awali liliafikiwa na rais Claudio Lolito. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ilikuwa imepishwa mpaka kufikia Julai 5 wawe angalau wameshasajili wachezaji wanne au watano ili kuimarisha kikosi lakini mpaka sasa hakuna yeyote aliyenunuliwa.
No comments:
Post a Comment