MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ujerumani, Mario Gomez anatarajiwa kukosa hatua zilizobakia za michuano ya Ulaya kufuatia kupata majeruhi ya msuli wa paja. Vipimo alivyochukuliwa baada ya mchezo wa robo fainali walioshinda dhidi ya Italia Jumamosi iliyopita vinaonyesha nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 amechanika msuli. Katika taarifa yake Chama cha Soka cha Ujerumani-DFB kilithibitisha taarifa hizo na kuongeza hataweza kushiriki michuano hiyo kwasasa. Viungo Sami Khedira na Bastian Schweinsteiger nao kuna hatihati ya kukosa mchezo wa nusu fainali utakaofanyika jijini Marseille Alhamisi hii kutokana na majeruhi yanayowasumbua.
No comments:
Post a Comment