Friday, July 1, 2016

RASMI: NEYMAR AANGUKA SAINI YA MKATABA MPYA BARCELONA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar amesaini rasmi mkataba wa miaka mitano na Barcelona ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka mwaka 2021. Kitenzi cha kumng’oa nyota huyo Barcelona kilikuwa ni kiasi cha euro milioni 200 lakini kinatarajiwa kuongezea na kufikia euro milioni 250 mpaka mkataba wake utakapokwisha. Mapema jana rais wa Barcelona, Josep maria Bartomeu alidokeza kufikia makubaliano katika mkutano na wanahabari kabla ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 hajathibitisha nia yake ya kubakia Camp Nou baadae. Neymar ambaye anatarajiwa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya michuano ya Olimpiki, amekuwa akihusishwa na tetesi kuwania na Manchester United na Paris Saint-Germain lakini sasa tetesi hizo zitazimika baada ya kusaini mkataba mpya.

No comments:

Post a Comment