MENEJA wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema ni wakati muafaka kwa Ryan Giggs kuondoka katika klabu hiyo na kuongeza ana nafasi kubwa ya kufanikiwa akatika kazi yake mpya ya ukocha. Giggs mwenye umri wa miaka 42, aliamua kuondoka baada ya kupita miaka 29 akiwa United, kufuatia meneja mpya Jose Mourinho kuamua kutomjumuisha katika benchi lake la ufundi. Ferguson alidai pia Mourinho ambaye alikuwa hasimu wake wa kitambo alikuwa yuko sahihi kuamua kumchukua mtu wake ambaye ni msaidizi wake wa kipindi kirefu Rui Faria. Akihojiwa Ferguson mwenye umri wa miaka 74, amesema anadhani ni muda muafaka kwa Giggs kutoka, kujisimamia mwenyewe na kukubali changamoto.
No comments:
Post a Comment