KLABU ya Manchester City imetangaza kumsajili rasmi kiungo chipukizi mwenye umri wa miaka 19 Oleksandr Zinchenko kutoka FC Ufa ya Urusi. Chipukizi huyo aliibuka katika kikosi cha kwanza cha Ufa msimu huu na kufanikiwa kupata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Ukraine huku akicheza mechi zote tatu za michuano ya Ulaya. Nyota huyo pia alijizolea jina nchini kwao kwa kuwa mchezaji mdogo zaidi katika taifa hilo kufunga bao akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Andriy Shevchenko, kwa bao alilofunga katika mchezo walioshinda 3-2 dhidi ya Romania Mei mwaka huu. Zinchenko aliondoka Shakhtar Donetsk mwaka 2015 na sasa anajikuta akifanya kazi na City chini ya Pep Guardiola ambaye tayari ameshawanasa Ilkay Gundogan, Aaron Mooy na Nolio.
No comments:
Post a Comment