WAKALA wa Olivier Giroud, Michael Manuello amebainisha kuwa mteja wake yuko tayari kuondoka Arsenal kwa dili la kubadilishana na Gonzalo Higuain. Taarifa kutoka nchini Italia zinadai, meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana matumaini ya kukubaliwa ofa ya paundi milioni 50 pamoja na Giroud na Napoli ili aweze kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina kufuatia kumkosa Jamie vardy. Higuain amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Ligi Kuu toka alipoondoka Real Madrid na Manuello amesisitiza mteja wake hawezi kumzuia Muargentina huyo. Manuello amesema kama Arsenal wakimtaka Giroud aondoke hawatakuwa na hiyana kuhusu hilo kwani anaamini Napoli ni timu nzuri na mteja wake huyo ataifurahia.
No comments:
Post a Comment