Tuesday, July 12, 2016

HENRY AKATAA KIBARUA ARSENAL.

NGULI wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry ameondoka katika klabu hiyo baada ya kukataa kibarua cha kukinoa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 18. Henry mwenye umri wa miaka 38, alikuwa amepewa ofa ya kibarua hicho na meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger ambaye alimuhabalisha kuwa hataweza kuchanganya na kibarua chake cha sasa cha uchambuzi katika luninga. Mkongwe huyo ambaye ndiye mfungaji bora wa wakati wote wa klabu hiyo, ambaye ana leseni daraja A ya ukocha kutoka Shirikisho la Soka Duniani-UEFA, anadaiwa kuwa hayuko tayari kuachia nafasi yake ya uchambuzi. Nahodha wa zamani wa Arsenal, Tony Adams mwenye umri wa miaka 49, anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo ya kikonoa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 18 cha Gunners.

No comments:

Post a Comment