KLABU ya Barcelona imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Lyon Samuel Umtiti baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kukubali kusaini mkataba wa miaka mitano Camp Nou. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amesajiliwa na klabu hiyo kwa kitita cha euro milioni 25 ambacho kina kitenzi cha euro milioni 60 katika mkataba wake. Umtiti aliibuka katika kikosi cha kwanza cha Lyon mwaka 2011 na kuja kucheza mechi 170 kwa klabu hiyo akishinda mataji mawili ya Kombe la Ufaransa na lile la Super Cup akiwa na klabu hiyo. Nyota huyo pia amewahi kutwaa taji la Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2013, na tayari amekichezea kikosi cha wakubwa mara tatu akicheza dakika zote tisini katika mechi dhidi ya Iceland, Ujerumani na baadae fainali ya michuano ya Ulaya dhidi ya Ureno. Umtiti anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na kusaini mkataba wake Ijumaa hii.
No comments:
Post a Comment