KLABU za Ligi Kuu zinadaiwa kutumia kiasi cha karibu paundi milioni 300 katika wiki ya kwanza toka kufunguliwa kwa dirisha usajili la majira ya kiangazi. Kulinganisha na mwaka jana, kiasi cha paundi milioni 870 ziliztumika katika kipindi cha wiki tisa katika usajili wa kiangazi mwkaa jana. Mchambuzi wa masuala ya kibiashara, Deloitte anategemea kiwango hicho kupanda na kuzidi paundi bilioni moja kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Agosti 31 mwaka huu. Mkataba wa mpya wa paundi bilioni tano kwa ajili ya matangazo ya luninga, ambao unaanza msimu huu ndio unatajwa kuwa utachangia kiwnago hicho kupand kutokana na mgao vilabu watakaopata. Kila klabu inaweza kutegemea kupata kati ya kiasi cha paundi milioni 30 au 50 kutoka katika Ligi Kuu msimu wa 2016-2017 ikiwa ni matokeo ya mkataba wa matangazo ya luninga ambayo Sky wamelipa.
No comments:
Post a Comment