MAOFISA wawili kutoka kwa mabingwa wa soka wa Sudan Kusini, Atlabara wameauawa katika mapigano mapya yaliyozuka nchini humo. William Batista na Leko Nelson walikuwa katikati ya vurugu hizo zilizozuka katika mji wa Juba ambapo majeshi yanayomtii rais wa nchi hiyo Salva Kiir nay ale yanayomtii makamu wa kwanza wa rais Riek Machar yaliporushiana risasi. Rais wa Chama cha Soka cha nchi hiyo, Chabur Goc alithibitisha taarifa hizo na kutoa pole kwa familia kwa kuwapoteza wapendwa wao. Majeshi yanayomtii Kiir na yele ya Machar yalianza kurushiana risasi katika mitaa ya mji wa Juba wiki iliyopita. Mahusiano kati ya viongozi hao wawili yamekuwa ya mashaka toka Sudan Kusini ilipopata uhuru wake kutoka Sudan mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment