Monday, July 11, 2016

SOUTHAMPTON MBIONI KULINASA KIUNGO LA BAYERN.

KIUNGO wa Bayern Munich, Pierre-Emile Hojbjerg anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Southampton. Nyota huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 20, anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo ya Ligi Kuu kwa kitita kinachokadiriwa kufikia paundi milioni 12.8. Hojbjerg alipelekwa kwa mkopo Schalke msimu uliopita na nafasi yake kurudi katika kikosi cha kwanza cha Bayern inaonekana kuzidi kuwa finyu kufuatia kusajiliwa kwa Renato Sanchez. Taarifa kutoka Bayern zinadai kuwa nyota huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo Southampton ambayo tayari imeshamsajili Nathan Redmond kiangazi hiki.

No comments:

Post a Comment